UTAFITI:NYANYASAJI WA KINGONO BADO NI TATIZO NCHINI TANZANIA
Utafiti wa uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu nchini Tanzania (LHCR) na kuutoa katika ripoti yake ya Haki za
Binadamu na Biashara ya Mwaka 2013 umegundua kuwa kwa upande wa haki za
kinjinsia,unyanyasaji wa kingono umefikia asilimia 28.3 nchini Tanzania.
Japokuwa unyanyasaji wa kijinsia makazini unaonekana
kupungua kutokana na kuongezeka kwa ufahamu wa haki za Binadamu bado
ukandamizaji wa namna mbalimbali umefikia asilimia 49 na asilimia 10 ya
wafanyakazi wa kike katika makampuni ndio waliopewa likizo ya uzazi.
Ripoti hiyo iliyotolewa mapema juma hili jijini Dar es
salaam imetokana na utafiti kwenye mikoa 15 ya Tanzania bara ambapo watafiti 30
walihusika katika kukusanya takwimu mbalimbali toka kwa watu zaidi ya 1,000
,makampuni 153 na ofisi 121 za serikali zilitoa taarifa mbalimbali.
Maeneo yaliyohusika na ripoti hiyo ni Haki za Ajira,Haki za
Ardhi,Kodi,Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii na Serikali,Haki za Mazingira na
Haki za Kijinsia.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa ni sehemu ya mpango mkakati wa
LHCR mwaka 2013 hadi 2018 katika kufuatilia uwajibikaji wa makampuni kwa
viwango vya ndani na vya kimataifa kwenye haki za kiuchumi,kijamii na
mazingira.
Post a Comment