MAKANISA YA WAADVENTISTA WASABATO ARUSHA WAENDESHA HUDUMA ZA KIJAMII NA KIROHO KATIKA GEREZA
Zaidi ya watoto 30 katika Gereza la watoto lijulikanalo kwa jina la Home Center lililoko Unga Ltd Arusha wanapata mafunzo ya kiroho kutoka kwa
wainjilisti na Idara ya Dorkasi ya kanisa la Waadventista Wa Sabato Njiro
jijini Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Muinjilisti Gerald Nyafanga wa Kanisa
la Waadventista Wa Sabato Njiro anayeendesha masomo na maombi katika
Gereza hilo amemwambia mwandishi wa habari hii asubuhi ya leo kuwa kuna umuhimu wa kuongeza nguvu zaidi ya
huduma za kiroho katika kitengo hicho na vingine vinavyofanana na hivyo
ili kuikoa jamii na matendo mabaya lakini pia kuifanya jamii ya watu hao
kuwa na amani pia
tumaini juu ya Mungu.
Zaidi ya maombi na mafunzo hayo watoto hao pia hupata misaada
mbalimbali kutoka kwa kanisa hilo ikiwa ni pamoja na vyakula,sabuni,
mafuta,pia wanapata nafasi ya kufanya mijadala mbalimbali ihusuyo Biblia,madhara ya madawa ya kulevya,ubaya wa uhalifu kwa Mungu na kwa
jamii inayozunguka.
Kanisa hilo pia limeanzisha darasa la muziki katika Gereza hilo darasa ambalo lina ongozwa na kiongozi wa muziki wa Kanisa hilo la Waadventista Wa Sabato Njiro.
Mbali na hayo wafungwa pamoja na viongozi wa gereza hilo la watoto wameonyesha kuyapenda mafunzo na wameeleza kuwa yatakuwa ni msaada mkubwa na chachu katka kuitengeneza jamii hiyo iweze kubadili mwelekeo uliokuwa mbaya na kumwelekea mungu wa mbinguni hasa wanapoendesha mijadala kuhusu namna ya kuacha madawa ya kulevya kwani ndilo tatizo kubwa kwa sasa linalowakabili vijana llikiwemo la ulevi, na ngono.
Mafunzo hayo hufanyika kila siku ya jumatano ya kila juma.
Na.Abel Kinyongo
Post a Comment