MTANGAZAJI

TAFITI:KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LINA WANAWAKIKE WENGI KULIKO WANAUME

 Tafiti zimeonyesha kuwa kanisa la Waadventista Wasabato linaidadi kubwa ya washiriki ya wanawakike ikilinganishwa na wakiume.

 Hayo yameelezwa na mmoja wa makamu wa Rais wa Kanisa la Waadventista Wasabato ulimwenguni Daktari Mchungaji Benjamini Schoun katika ukumbi wa Advent Hill uliopo makao makuu ya kanisa la Waadventista Wasabato ya Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi katika warsha ya teknolojia ya habari na mawasiliano

Daktari Schoun ameongeza kuwa,mbali na idadi ya wanawakike kuwa kubwa,idara ya shule ya sabato imeendelea kufanya vizuri sana ikilinganishwa na idara mbalimbali za kanisa.Hata hivyo  imeonekana ni idadi ndogo ya washiriki wanao wapeleka watoto wao kupata elimu katika shule za kanisa.

 Warsha ya teknolojia ya habari na mawasiliano imemalizika jana iliwakutanisha wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Ulaya, hata huku wajumbe wakionyesha kufurahishwa na wakufunzi mbalimbali walio simama katika zamu zao. 

 Na. Miller James-Nairobi

1 comment

Anonymous said...

Habari njema ingependeza kutoa takwimu kwa habari hiyo. Isiishie namba tu bali hata utambuzi wa mchango wao katika uinjilisti na kazi za makanisa mahalia

Mtazamo News . Powered by Blogger.