RIPOTI YA JAMII PRODUCTION KUHUSU KUPOTEA KWA NDEGE YA MALAYSIA
Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011. Photo Credits: PressTv |
Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea
tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana
wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Machi 22, 2014
Post a Comment