MTANGAZAJI

BINAGI SACCOS YAWANUFAISHA WANANCHI WA BINAGI,TARIME

Wanachama wa chama cha kuweka na kukopa wilayani Tarime kata ya Binagi tarafa ya inchage mkoani Mara BINAGI SACCOS wameushukuru mradi wa DASIP kwa kuwapatia elimu juu ya uwezo wa kuweka na kukopa.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti wanachama hao wamesema kuwa kabla ya chama hicho kuanzishwa mwaka 2003 maisha yao yalikuwa duni lakini hivi sasa wameboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kuwasomesha watoto ,kujenga nyumba na ununuzi wa vyombo ya usafiri .


Naye meneja wa BINAGI SACCOS hiyo Bwana Patrice Mang`iti amesema kuwa wakati wa uanzishwaji wa SACCOS hiyo walikuwa na jumla ya wanachama 260 huku wakiwa na shilingi 260,230 lakini mpaka sasa wanajumla ya wanachama 1289 na kiasi cha akiba ya shilingi milioni 232.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.