WAKAZI WA VIJIJI WILAYANI BUNDA WAENDELEA KUGOMA KUPISHA NJIA YA WANYAMA WA SERENGETI
Wakazi
wa vijiji vitatu vya Serengeti,Nyatwali na Tamau wilayani Bunda
wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutotaka kuhama ili kupisha njia
ya kupeleka wanyama kutoka hifadhi ya Serengeti kunywa maji ya Ziwa
Victoria.
Serikali wilayani Bunda kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA imekuwa ikiwataka wakazi hao kulihama eneo hilo ili ijengwe njia ya kupitishia wanyama kwa lengo la kukuza utalii jambo ambalo limekuwa likipingwa mara kwa mara na wakazi hao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema ,badala ya kuwahamisha na kuwaingiza katika usumbufu, TANAPA inaweza kujenga mabwawa ndani ya eneo la hifadhi hiyo na hivyo kuwawezesha wanyama hao kunywa maji kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Bunda Bwana Joshua Mirumbe amesema kuwa serikali haina mpango wa kuwahamisha na badala yake inaangalia uwezekano wa kulifanya eneo hilo kuwa moja ya vivutio vya utalii vitakavyoiongezea mapato serikali.

Post a Comment