MTANGAZAJI

WAADVENTISTA WA SABATO WATAKIWA KUWA NA MTAZAMO CHANYA WA INJILI KATIKA MAJIJI

Washiriki wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato jijini Mwanza wametakiwa kuwa na mtizamo chanya wa injili katika majiji makubwa.

Akizungumza na washiriki wa mitaa mbalimbali katika maandalizi ya mahubiri ya miji mikubwa yaani (Big Cities) ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Jijini Mwanza, Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Division ya nchi za Afrika Mashariki na Kati Mchungaji Blasious Ruguri amesema kuwa,kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaohama vijijini kuja mijini hivyo kanisa linapaswa kuwa na mipango madhubuti ya kuwafikia watu hao.


Mahubiri ya miji mikubwa yanayojulikana kwa jina la Big city yanatarajiwa kufanyika jijini Mwanza ,Dar es salaam na Arusha mapema mwaka huu.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.