MTANGAZAJI

POLISI WAKAMATA WATUHUMIWA WA KUSAFIRISHA WATOTO

Sakata la biashara ya binadamu lililoibuka kwa kasi nchini limeanza kufanyiwa kazi na serikali baada ya Jeshi la Polisi Kikosi cha Maji kuwatia mbaroni mawakala 5 ambao ni wanawake, wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Maji, Mboje Kanga, akizungumza na NIPASHE jana kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na jeshi hilo kukabiliana na tatizo hilo, alisema mawakala waliokamatwa ni wakazi wa Zanzibar na kwamba hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi yao.

Kamanda Kanga ambaye hata hivyo, hakutaja majina ya mawakala hao, alisema walikamatwa kati ya Januari 23 na 24, mwaka huu wakiwa na watoto watano ambao waliwanunua kutoka mikoani.

Alisema watoto ambao ni wanafunzi wa shule za msingi walikamatwa wakitaka kusafirishwa na mawakala hao kwenda Zanzibar, umri wao ni kati ya miaka 14 na 15 na walitoka katika wilaya za mikoa ya Ruvuma, Tabora na Mtwara.

Aliongeza kuwa katika mahojiano na watoto hao walisema walipata ridhaa ya kuchukuliwa na mawakala hao ambao haijafahamika baada ya kusafirishwa kwenda Zanzibar wangepelekwa katika nchi gani.


 Wastani wa watoto kati ya 5 -10 wa kike na wachache wa kiume, hufika katika Bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusafiri kwenda Zanzibar kila siku. Uchunguzi  huru wa NIPASHE umebaini kuwa Januari 23, mwaka huu waliwatilia shaka na polisi na kuzuiwa kusafiri ni watoto wanne ambao walifunguliwa jalada la upelelezi kituo cha Polisi Maji ambazo ni MUD/RB/40/2013 na MUD/RB/36/2013.
Chanzo:Wavuti

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.