MTANGAZAJI

TAARIFA KUHUSU HALI YA MHARIRI WA GAZETI ALIYEPIGWA RISASI TANZANIA Kwa niaba ya Kampuni ya Business Times Limited, napenda kuwataarifu kwamba kikao cha kujadili hali na mwenendo mzima wa Mhariri mwenzetu Mnaku Mbani(Pichani) ndio kimekwisha na kuahidi kutoa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari ili kuelezea uhalisia wa tukio zima na nini kinaendelea kwa faida ya vyombo vyote vya habari pamoja na msimamo mzima wa Business Times Limited.
Tafadhali tunaomba uvumilivu wenu wakati tunaendelea kufuatilia taratibu zote.
Asanteni na poleni,
Imma Mbuguni

Pichani ni Mnaku Mbani Lukanga (Mhariri wa gazeti la Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo  aliophamishwa kutoka hospitali ya Temeke alikolazwa jana mara baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi hapo jana usiku katika mtaa wa Lugoda akiwa anaelekea nyumbani kwake Mbagala usiku wa saa mbili jioni.
Katika tukio hilo, alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi.
Baadhi yao walitolewa risasi na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto. Bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.