MTANGAZAJI

MHE JACKSON MAKWETA AFARIKI DUNIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA

Serikali ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta
kilichotokea Novemba 17,2012 saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango
ya mazishi zitatolewa baadaye.

Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo
Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.

Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.