UNAOMBWA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYU
MILIONI sita zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto Selemani
Said (1), ambaye anajisaidia haja kubwa kupitia utumbo mkubwa huku ukiwa
nje ya tumbo lake imeleezwa.
Akizungumza na wandishi wa habari Katika Ukumbi wa Idara ya Habari
(Maelezo),jijini Dar es Salaam leo, mama wa mtoto huyo, Veronika Laurent
ambaye ni Mkazi wa Bunju, alisema mtoto huyo alizaliwa huku akiwa na
sehemu ya kutolea haja kubwa lakini cha kushangaza, haja kubwa ilikuwa
ikitokea mdomoni.
Alisema msaada wa fedha hizo utasaidia katika kumfanyia operesheni
mtoto huyo ambaye kwa sasa anaishi akiwa katika mateso makubwa.
Veronika alisema hivi sasa yeye pamoja na mwanaye huyo wanaishi
maisha ya kubahatisha baada ya baba wa mtotohuyo kuitelekeza familia
hiyo kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto huyo.
“Mimi ni nachoomba ni msaada wa fedha ili niweze kumpeleka kwenye
matibabu kwani sina msaada wowote,ukichukulia wazazi wangu kufariki na
hivi sasa naishi kwenye nyumba ya mwenyekiti wa Mtaa wa Bunju wilayani
Kinondoni jijini baada ya kushindwa kupangisha chumba kwani sina kazi
yeyote”alisema.
Aidha, alisema hadi utumbo wa mtoto huyo kutoka nje, ni baada ya
kufanyiwa operesheni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo hata
alipompeleka tena kwa ajili ya matibabu alikosa ushirikiano kutoka kwa
madaktari na wahudumu wengine.
Alisema kwa yeyote ambaye yuko tayari kumsaidia anaweza wasiliana
naye kwa kupiga simu namba o715 83 77 00, na namba ya mwenyekiti huyo wa
mtaa 0656780236.
Veronika ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro eneo la Kijiji cha
Uru,Moshi ambaye alimzaa mtoto huyo na mwanamme aliyemtaja kwa jina la
Abdalah Said, kabilake makonde mfanyabiashara wa viatu Ubungo.
Post a Comment