MTANGAZAJI

VIFO VYA MAPEMA BARANI AFRIKA! KWA NINI?

Mazishi ya hayati rais John Atta Mills
Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani.
Tangu mwaka 2008, hili limefanyika mara kumi na tatu kote duniani -lakini kumi kati ya viongozi hao wamekuwa marais wa nchi za afrika.

Kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?
Makundi makubwa ya watu walikusanyika kushuhudia jeneza la hayati waziri mkuu wa Ethiopia meles Zenawililipokuwa likipitishwa katikati mwa mji mkuu Addis Ababa, mnamo siku ya Jumanne wiki iliyopita. Alifariki akiwa na umri wa miaka 57, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mapema mwezi huu, maelfu ya wananchi wa Ghana walihudhuria mazishi ya hayati rais, John Atta Mills, aliyefariki ghafla akiwa na umri wa miaka 68.

Miezi minne kabla ya kifo cha Atta Mills, siku ya kitaifa ilitangazwa nchini Malawi kuwezesha maelfu ya watu kuhudhuria mazishi ya hayati rais Bingu wa Mutharika, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 78 kutokana na mshtuko wa moyo.

Na mnamo mwezi Januari, rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha, alifariki katika hospitali ya kijeshi mjini paris baada ya kuugua kwa muda mrefu. Alikuwa na umri wa miaka 64.

Kwa hivyo viongozi wanne wa Afrika wamefariki mwaka huu pekee . Bila shaka ni pigo kwa nchi husika na huzuni kubwa kwa familia za viongozi hao. Lakini je mwandishi wa habari atafsiri vipi matukio haya?

"Kila usiku Napata simu nyingi kutoka kwa watu wengi kuniambia rais wa Afrika ameaga dunia" anasemaSimon Allison, mwandishi habari wa mtandao wa habari wa Daily Maverick nchini Afrika Kusini. "Kwa nini viongozi wengi wa Afrika wanafariki sana wakati huu? anahoji Simon.

Swali hili bila shaka linasababisha tathmini ya maisha ya viongozi hao.
" Ukitafakari kidogo orodha ya viongozi wa Afrika waliofariki bila shaka ni ndefu'' anasemaAllison. Tangu mwaka 2008, viongozi 10 wa Afrika wamefariki wakiwa madarakani.

Viongozi wengine wa Afrika waliofariki wakiwa madarakani ni pamoja na Muammar Gaddafi akiwa na miaka 69. Aliauawa wakati wa mapinduzi ya kiraia nchini Libya Oktoba mwaka 2011

Aliyekuwa rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua aliaga akiwa na miaka 58 mwezi Mei mwaka 2010 kutokana na maradhi ya figo pamoja na moyo.

Omar Bongo wa Gabon akiwa na miaka 73 alifariki mwaka 2009
Raia wa Guinea Bissau president, J B Vieira umri wa miaka 69 aliuawa mwezi Machi mwaka 2009

Rais wa Guinea Lansana Conte aliaga akiwa na miaka 74 mwaka 2008, kutokana na sababu zisizojulikana.
Aliyekuwa rais wa Zambia , Levy Mwanawasa akiwa na miaka 59 mwaka 2008, kutokana na kiharusi.

Bila shaka ni kweli kuwa viongozi wengi wa Afrika wanaaga dunia wakiwa wangali madarakani kuliko katika bara lengine lolote duniani. Katika kipindi hicho ni viongozi watatu pekee waliofariki wakiwa wangali madarakani kwingineko duniani.

Kim Jong Il wa Korea kaskazini , rais wa Poland, Lech Kaczynski, aliyefariki katika ajali ya ndege na David Thomson wa Barbados, aliyefariki kutokana na saratani.

Jibu la wazi ni kuwa marais wa Afrioka ndio wakongwe zaidi kuliko marais wa mabara mengine.Tathmini inayotolewa hapa ni kuwa waafrika wanapenda wenyewe kuwa na viongozi wazee kwani kulingana na utamaduni , wanapata heshima kubwa kutoka kwa jamii.

Muda mrefu zaidi ambao marais wa Afrika wanaweza kuishi inakadariwa kuwa miaka 61 sawa na bara Asia. Viongozi wa bara la Afrika, umri wao unakakadiriwa kuwa miaka 55 wakati barani Afrika rais mkongwe zaidi anakadiriwa kuwa na miaka 59.

Lakini kitu kingine cha kutafakari ni umri mrefu zaidi wanaoishi watu wa bara hilo ikikadiriwa kuwa chini sana barani Afrika ikilinganishwa na mabara mengine kama Uropa, Amerika ya kusini na barani Asia.

Sababu kuu hapa ikiwa ni janga la ukimwi, na pia miundo msingi duni ya afya ambayo inachangia idadi kubwa ya vifo hasa miongoni mwa watoto wachanga.
Lakini umaskini katika maisha ya ujana na kwa watoto wachanga pia zinaathiri kubwa katika umri wa mtu kulingana na daktari George Leeson wa chuo kikuu cha Oxford.

"marais wa Afrika kabla ya kuchaguliwa huenda waliishi maisha ambayo sio mazuri sana na bila shaka hilo litaathiri maisha yao uzeeni'' anasema daktari Leeson.

Kwa hivyo wakati wanapoingia madarakani, licha ya kuwa sasa wanaishi maisha ya kifahari zaidi kuliko siku zao za utotoni, bado athari za maisha duni walipokuwa wachanga huwaandama

Lakini hii haimaanishi kuwa viongozi wote wa Afrika waliishi maisha duni walipokuwa wadogo. Kuna mambo mengine chungu nzima ya kuzingatia. Mfano, siasa, dhana kwamba, viongozi wa afrika wanapenda kung'ang'ania madarakani, hadi watapofariki. Lakini dhana hii ingali kuthibitishwa.

Lakini kunao viongozi waliong'ang'ania madaraka hadi wakafa, kama vile Omar Bongo, Conte na Gaddafi, kulingana na tathmini mbali mbali. Lakini wengine kama Meles Zenawi waligandia tu madarakani , kwa sababu kama Zenawi, alikuwa na miaka 57 pakee.

Hata hivyo ni muhimu kujua kuwa tathmini hii ni ya viongoiz tu waliofariki wakiwa ofisini tangu mwaka 2008.

Chanzo:BBC

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.