MTANGAZAJI

BABU WA LOLIONDO KUSHITAKIWA!!!!!!!!

Iwapo atapatikana na hatia:
  • Vipi kuhusu mawaziri na vigogo wa serikali waliokuwa wakimiminika Loliondo huku wakiifagilia dawa hiyo kwamba ilikuwa imewasaidia na hivyo kuendelea kuchochea moto wa tiba hiyo?  Hawahusiki kwa namna yo yote na "utapeli" huu?
  • Vipi kuhusu ripoti ya "wataalamu" iliyosema kwamba kikombe cha babu kilikuwa ni tiba bomba? Vipi kuhusu wagonjwa waliokuwa wakisimama na kuitetea dawa hiyo kwamba ilikuwa inatibu? Vipi kuhusu watoa vikombe wengine waliokuwa wamechipuka sehemu mbalimbali nchini? Nao watashtakiwa?  
Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ wa Samunge, Loliondo, Arusha, atapanda kizimbani kukabili kesi za madai na jinai, hii ni kwa mujibu wa wakili maarufu, Mabere Nyaucho Marando.

Wakili huyo alisema, endapo mahakama itamkuta na hatia ya kutenda jinai, Babu Ambi, anaweza kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka saba jela.Marando alisema, kesi ya jinai ambayo Babu Ambi anafunguliwa ni ile ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kwamba aliwahadaa watu kuwa dawa yake inatibu, wakati hakuna mtumiaji aliyepona. 

Aliongeza kuwa kesi ya madai, inafunguliwa kwa sababu anatakiwa alipe fidia za watu waliopoteza maisha na wote waliosafiri kutokana sehemu mbalimbali wakitumia gharama kubwa kwa dawa isiyotibu.
    Chanzo:Matondo blog na Global Publishers

    2 comments

    Anonymous said...

    wajinga ndio waliwao...

    Anonymous said...

    Babu kashtakiwa! Vp Bibi wa Tabora, Kaka wa Mbeya na wengi waliofuata janja ya Babu ya tiba cha Kikombe?
    Hizi ni siku za mwisho bwana!!

    Mtazamo News . Powered by Blogger.