MTANGAZAJI

AMBASSADORS OF CHRIST WAKANUSHA KUWEPO DODOMA

Sara Uwera akiwaongoza waimbaji wa Ambassadors of Christ
Waimbaji wa Ambassadors of Christ wanapenda  kuwataahadharisha watanzania hasa wa mkoa wa DODOMA ya kuwa habari ya kuwa kwaya hiyo ya Kanisa la Waadventista Wasabato Remera itakuwepo siku ya Disemba 25,2011 si ya kweli. 
Akizungumza na blog hii Mwalimu wa Kwaya hiyo Sozzi Joram amesema ifahamike ya kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hizo na Ambassadors of Christ wamesikitishwa sana na uvumi huo. 
Sozzy aliyeanza kuifundisha kwaya hiyo mwaka 1998 amesema kuwa Ambassadors of  Christ ni kwaya ya Kanisa na haijapata mwaliko wowote wa kushiriki tamasha lolote hapo DODOMA kwa kufuata taratibu za kanisa la Waadventista wasabato na anasisitiza kuwa kwaya hiyo haitakuwepo siku hiyo.

1 comment

Anonymous said...

Good!

Mtazamo News . Powered by Blogger.