MTANGAZAJI

UMURISA VYONNE KUFUNGA PINGU ZA MAISHA

Umurisa Yvonne akiwa na mumewe mtarajiwa katika sherehe ya maandalizi ya harusi hivi karubuni huko Rwanda
Mwimbaji wa Kwaya ya Ambassadors Christ ya Rwanda na ambaye ameimba solo katika wimbo wa Kwetu Pazuri kwa Kiswahili na KinyarwandaUmurisa Yvonne  atafunga pingu za maisha Agosti 14 mwaka huu.

Pia kutakuwa na Tamasha la kwaya hiyo huko Kigali,Agosti 17 mwaka huu ni kwa ajili ya watu maarufu (VIP) katika ukumbi wa hoteli ya Serena  Agosti 21 itakuwa ni tamasha kubwa katika uwanja wa taifa wa Amahoro. Mwimbaji mwingine wa kwaya hiyo Grace Kavalo ambaye aliumia mkono katika ajali amerudi tena hospital kwaajili ya upasuaji mwingine, mkono wake bado hajapona. 

Matamasha haya mawili ni kwa ajili ya kuchangia fedha, kwani deni hospitali kwa wagonjwa wote wanne waliumia kwenye ajali ya waimbaji hao mwaka huu nchini Tanzania ni faranga 25 milioni sawa na milioni  50 za Tanzania

Waimbaji wengine watakaokuwepo katika tamasha hilo ni Golden Gate na kwaya zingine 2 toka Uganda, Injili Family wa Congo, Acacia toka Tanzania, Israel toka Nairobi,Elshadai na Rehoboth Choir za Rwanda. Uwanja wa Amahoro utakuwa wazikuanzia saa 4 asubuhi.

4 comments

Anonymous said...

Namtakia Yvonne maisha mema yenye baraka tele,azidi kuwa baraka akimpendeza MUNGU na wanadamu pia.

BARIKIWA NA BWANA YVONNE.


Abraham Jesse
Kurasini.

Timba said...

i believe huyo ndugu kapata mke mwema God bless them!!

Anonymous said...

Jamani mmeoana furahi cheka kidogo basi... kama umelazimishwa....

Anonymous said...

I am happy for Yvonne and at the same time very sad.
Confession: I fell in love with her from the first day i saw her. Yvonne i had planned to look for you in Rwanda
Mr. Habimana, i know for sure you've found a very beautiful woman take care of her good.

Ralph,
Kenya

Mtazamo News . Powered by Blogger.