MTANGAZAJI

UJERUMANI YASITISHA KUTOA FEDHA ZA KUPAMBANA NA UKIMWI -TZ

WIZARA ya Maendeleo ya Ujerumani imetangaza kwamba itasitisha kutoa fedha kiasi cha euro milioni 200 ambazo hutolewa kila mwaka kwa  mfuko unaopambana na maradhi ya UKIMWI,kifua kikuu na
Malaria  duniani kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ufisadi.

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani, Dirk Niebel amesema katika taarifa yake kwamba,hatua hiyo inachukuliwa ili  maswali kadhaa muhimu yaliyojitokeza kuhusiana na kazi za shirika hilo ili yaweze kufanyiwa uchunguzi wa kina.


Hivi karibuni, vyombo vya habari viliarifu kuwa mamilioni ya dola katika shirika hilo yametumika vibaya na kwamba udhibiti wa kufuatilia michango inayotolewa ni mdogo au haupo kabisa.


Ujerumani ni nchi ya tatu inayotoa kiasi kikubwa cha fedha katika shirika hilo la kupambana na maradhi ya Malaria, UKIMWI pamoja na TB.

 Source: Dar Leo

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.