MTANGAZAJI

NAULI ZA DALADALA ZAPANDA NCHINI




Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imetangaza kupanda kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani.

 Meneja Mawasiliano kwa UMMAWA SUMATRA, David Mziray amesema nauli za daladala zitaongezeka kwa Sh. 50 na wanafunzi watalipa Sh. 150 kwa kila safari.

Kwa sasa, nauli ya chini ni Sh. 250 na ya juu ni Sh. 450, hivyo kwa mabadiliko hayo, nauli ya chini itakuwa Sh. 300 na ya juu Sh500 kwa safari za ndani ya Dar es Salaam.

Amesema Wajumbe wa Bodi ya SUMATRA waliokutana Januari 31 mwaka 2011 jijini Dar es Salaam, wamekubali na kuamua kupitisha maombi ya kupandisha nauli.

Hata hivyo, katika tangazo lililotolewa na SUMATRA jana, nauli hizo kwa watu wazima kwa Jiji la Dar es Salaam zitakuwa Sh. 27 kwa kilometa moja kwa watu wazima kutoka Sh. 22.9 za awali.

Sumatra imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo askari polisi wote na wanajeshi walio na sare za kazi hawatalipa nauli.

Tangazo hilo la SUMATRA limeeleza kuwa nauli mpya zitaanza kutumika Machi 10, 2011 na kuagiza wenye mabasi ya abiria kufuata maagizo mbalimbali yanayoambatana na mabadiliko hayo ya nauli.

Maagizo hayo ni pamoja na kila basi kuweka wazi idadi ya abiria litakalowabeba wakiwa wameketi na kusimama, makondakta na madereva kuvaa sare na beji zinazoonyesha namba ya gari wanalofanyia kazi pamoja na magari hayo kuwa na bima kwa magari yao na abiria.

 Toka Gazeti la Mwananchi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.