MTANGAZAJI

LIVE KUTOKA KWA BABU LOLIONDO


Kaimu mkuu wa Mkoa wa Arusha nchini Tanzania Raymond Mushi amesema ni vigumu kusitisha huduma ya tiba inayotolewa na Mch.Ambilikile Mwasapile( Babu wa Loliondo).

Kauli hiyo ya kaimu mkuu wa mkoa inafuatia agizo la serikali la kusitisha tiba hiyo ililolitoa kupitia Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii nchini Dr Haji Mponda.

Kabla ya taarifa hiyo ya serikali  Babu wa Loliondo alishaomba Serikali imsaidie kupata gari la kubeba dawa, vyombo vya kunywea, kuni na vyombo vikubwa vya kuchemshia dawa hiyo ili kukabili wingi wa wagonjwa wanaohitaji tiba hiyo.

Hizi ni picha kadhaa kutoka kwa mdau Humphery Soka za taswira huko Loliondo kwa babu, tuone jinsi watu na magari yalivyo mengi. Kwa kifupi toka Ijumaa mpaka jumatatu kulikuwa na magari kama 5000 yakiwa kwenye foleni, huku vitu vikipatikana n kwa bei ghali hata watu wakija wanatakiwa wawe na hela ya kutosha, maji na sehemu za kulala hakuna labda kama una gari lako ndiyo afdhali unaweza kwenda kutafuta maji lakini. pia ukalala kwenye gari lako.


Watu wanalala chini,vyoo navyo hakuna watu wanajisaidi kila mahali,serikali ingejitahidi waweke choo lasivyo kipindupindu kitakwenda tena kwa kasi ya hatari wewe fikiria kuziba pancha tu ni 10000, nyama ya kuchoma ya mbuzi ni shs 18000,maji ya kilimanjaro ni 3000 ya bombani 1000. Ajali hazijakosekana kuna hiyo picha ya Land cruizer ya grey ilianguka wakainyanyaua na magari yaliyochwa porini yameharibika ni mengi lakini kwa leo ni hayo tu mdau.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.