MTANGAZAJI

HATMA YA WATANZANIA WALIOKO NJE YA NCHI BUNGE LIJALO

HATMA ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi inatarajia kujulikana wakati wa kikao cha Bunge kinachotarajiwa kufanyika Aprili.

Uraia wa nchi mbili ni moja kati ya masuala yatakayotolewa majibu wakati wa Bunge hilo.
Hayo yalielezwa juzi usiku jijini Dar es Salaam, na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati akizungumza kupitia televisheni ya ITV.

Membe ambaye hakuzungumza kwa kina kuhusu suala hilo aliwataka Watanzania kuwa na subira.
Kwa mujibu wa Waziri huyo idadi ya Watanzania walioko nje inakadiriwa kufikia kati ya milioni 1.5 hadi 2.
“…Bado tunaendelea kuwatambua kwa idadi, lazima tufanye hivyo ili waweze kuleta fedha wanazotengeneza huko nje nyumbani kupitia jamaa zao mbalimbali hatimaye kuleta maendeleo,” alisema Membe.

Waziri huyo alisema pamoja na mambo mengine kuna matatizo mawili yanayotatiza, la kwanza ni kuwa si Watanzania wote wanaoweza kuruhusiwa kutuma pesa nchini kwani wanaoruhusiwa kufanya hivyo ni wale wanaotambuliwa na nchi yao na wengine hufanya hivyo kwa siri.

Kutoka:www.fotobaraza.me

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.