MTANGAZAJI

JE MAFANIKIO KWA WAAFRIKA NI SABABU YA KUHARIBIKA KWA NDOA?

Leo katika kipindi cha Sema na Jamii hapa Morning Star Radio 105.3 FM,Mada ilikuwa ni vipi mafanikio kwa baadhi ya  wanandoa barani Afrika yanaweza kuifanya ndoa iparanganyike?Haya ni maoni ya baadhi ya wasikilizaji waliotuma ujumbe mfupi wa maneno(sms):

1.       Ukweli inauma wanaume wamechangia lakini wanawake wananyanyasika kwani baba alikua na mali lkn mama hakuona raha ya zile mali mpaka baba alipofariki.
2.       Mtangazaji mada hiyo imenigusa sana kwan nilimsomesha mke  wangu  alipofanikiwa na kupata kazi nzur alibadilika  na kuanza kunidharau hadi kufikia hatua ya kuzaa mtoto nje ya ndoa,hali tuna watoto wawili hivi ndoa yangu ikokatika hatua ya mwisho...mimi ni gaqriel wa makondeko
3.       WANAUME WA KIAFRICA HUTAFUTA FARAJA NJE YA NDOA ZAO WAKIKOSANA NDANI,NIMESHAFUATWA NA MWANAUME WA AINA HIYO AKANIELEZA MTATIZO YA NDOA YAKE.
4.       MIMI NINA MFANO HAI KWANI BABA YANGU WALIHANGAIKA NA MAMA KWA NJIA YA KILIMO NASASA BABA NI TAJIRI MKUBWA PALE MWANZA LAKINI HAMJALI MAMA NA ALISHAOA BINTI MDOGO NA UKIZINGATIA KWA SASA NI WAZEE HAMKUMBUKI KWA CHOCHOTE.
5.       Mimi ninaumia kuona wanawake wanakandamizwa lkn wanaume wanaongoza kwa mabadiliko, nimewahi kukutana na baba mmoja anaonekana kua na wanawake wengi ukiangalia ama umri mkubwa hata mimi alinitongoza huku aki2mia mali zake kunishawishi.
6.       Maduhu,dah! Uwezi amin wanaume wengi ktk jiji il la dar siyo waaminifu kwan ukitaka kujua ili fuatilia wakati wake zao wanaujauzito/wamejifungua! Ndo wakati wao wa kujivinjal na vimwana.Duh! Hawana hata haibu jaman hebu hachen kwan ni dhambi kubwa.By jita boy
7.       Mimi ni kijana namshukuru Mungu kwan nina miaka 21 na cjawah kuingia kwenye mahusiano mpaka niingie kwenye ndoa pia nawashaur vijana wenzangu kujiepusha na mahusiano kabla ya ndoa.
8.       Kaka Maduhu mada hiyo imenigusa sana kwan nilimsomesha mke  wangu  alipofanikiwa na kupata kazi nzur alibadilika  na kuanza kunidharau hadi kufikia hatua ya kuzaa mtoto nje ya ndoa,hali tuna watoto wawili hivi ndoa yangu ikokatika hatua ya mwisho...mimi ni gaqriel wa makondeko
9.       HILO NI TATIZO KUBWA KTK NDOA,HATA MIMI LINANISUMBUA KWANGU,MUME WANGU ANAHISI NAMNYANYASA NA MSHAHARA WANGU.
10.   Wapendwa inategemea mlijengaje Upendo na Uhusiano wenu mwanzoni. Kama kipindi mwanaume alikuwa na kipato alikuwa jeuri kwa namna yoyote ile, basi atakapoishiwa mambo yatamgeukia. Ainess Baraka wa Luhanga
11.   Wengi we2 2najisahau kwamb hata bila kipato maish yanaendelea, weng 2mewekez katik maish ya dunian ambay yanamwish naitwa Raphael wa chuo kikuu dsm!

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.