MTANGAZAJI

TCRA YAONYA KAMPUNI ZA SIMU KUVUJISHA SIRI

Nimeona leo kwenye magazeti ya kiingereza tangazo hilo la onyo lakini matendo haya yamekuwa yanatokea mara kwa mara kwa miaka mingi nilitegemea kampuni za simu nazo pamoja na nyingine za mawasiliano kutoa matamko kuweza kuelezea suala hili kwa wateja wao lakini kampuni zote ziko kimya mpaka sasa hivi .

Kampuni za huduma za simu na nyingine za mawasiliano zinatakiwa kujua kwamba tume ya mawasiliano tanzania haiwezi kufanya kazi hii peke yake inahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau wengine pia ili waweze kufanya kazi vizuri na kutenda haki kuliko hivi kunyamaza .

Pia TCRA inatakiwa kuweka fomu ya malalamiko kwenye tovuti yake ili watu waweze kutumia fomu hiyo kutoa malalamiko yao mbalimbali ili iwe rahisi kuweza kufikisha ujumbe .

                                    
Yona Fares Maro  
 I.T. Specialist and Digital Security Consultant

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.