DINI ZETU NA MAKEMEO KWA SERIKALI
Duh kwenye zile siku wanazoziita sikukuu (utafikiri kuna siku ndogo, kwangu zote ni sawa tu), tumekuwa tukisikia viongozi wa dini na makemeo yao yenye shibe kwa serikali! ndugu, ukisikiliza vyombo vya habari katika siku hizi unaweza dhani serikali yetu inaongozwa na watu gani sijui mimi
kila kiongozi wa dini huwa wanaikemea serikali as if ndio ibilisi wafanyayo kazi ya kumkemea. utasikia tunataka amani, mara ufisadi mara nini sijui. utafikiri viongozi wetu wa dini hizi ni wema sana au labda wanaonyesha wema wao kupitia kwa viongozi wa dini hizi
umefika wakati wa viongozi wa dini na dini zetu kujitathmini kila siku zao kuu ili kuona walipo toka, walipo na wanapokwenda! viongozi wa dini wanaikemea serikali wakati serikali inaongozwa na wafuasi wa dini zenyewe. serikali inaposhindwa kufanya kitu fulani au ikadondokea kwenye upotevu ni vyema wakajua kuwa dini ndo imepotea na sio serikali, si viongozi wentu wanadini na huapa kwa misahafu ya dini zao?
kila mwaka hali inabadilika, vijana hawaendi kwenye ibada tena wanaingia kwenye ulevi, matumizi ya bangi, madawa ya kulevya na ngono holela kama sio hatarishi. waumini wa dini hizo nao hudondokea katika ifisadi na kutumia vibaya madaraka, harafu eti viongozi hawa kwenye sikukuu wanaikemea serikali na kuipangia majukumu kibao! ili waonekane wanavyowajali wafuasi wao?
imefika wakati sasa wachunga kondoo wetu hawa wawe na tabia ya kujitathimini kila wakati badala ya kuipangia kazi serikali. wajiangalia jinsi wafuasi wao watiifu wanavyozidi kutumia nafasi zao vibaya, waangalie jinsi waumini wao wanavyo iba pesa na kuileta kama sadaka kwenye nyumba za ibada, watathimini mienendo ya waumini na hata viongozi wa dini inavyozidi kuwa ya kumfuata yule mwovu na hivyo kupanga mikakati ya kujenga jami imara!
lakini watawezaje kufanya hivyo wakati wao wenyewe (viongozi wa dini, wahubiri, waongoza ibada nk) wanazidi kutumbukia majaribuni kila uchao? labda iwepo taasisi ya kuwasema pia hawa ili wajitathimini, wasiangali boriti katika jicho la serikali bali waone kibanzi kwao kwanza na kukishughulikia
Na. Kamala Lutatinisibwaumefika wakati wa viongozi wa dini na dini zetu kujitathmini kila siku zao kuu ili kuona walipo toka, walipo na wanapokwenda! viongozi wa dini wanaikemea serikali wakati serikali inaongozwa na wafuasi wa dini zenyewe. serikali inaposhindwa kufanya kitu fulani au ikadondokea kwenye upotevu ni vyema wakajua kuwa dini ndo imepotea na sio serikali, si viongozi wentu wanadini na huapa kwa misahafu ya dini zao?

Post a Comment