MTANGAZAJI

WAZO LA LEO

Na Maggid Mjengwa,

UKITAKA kumjua Mwafrika, basi, mwangalie siku anapohama. Ndivyo tulivyo. Hata kwenye uongozi, ni hivyo hivyo. Mwangalie kiongozi wa Afrika anapoingia na anapotoka kwenye madaraka.

Ndio, hana tofauti sana na Mswahili anayehama kutoka Mwananyamala kwenda Magomeni. Mswahili wa Mwananyamala, hata kama atahakikishiswa, kuwa anakohamia Magomeni vyumba vyote vina taa za balbu na pazia za madirishani na milangoni, bado, Mswahili huyu atahakikisha, kabla ya kuhama, anang’oa balbu na pazia zote kutoka nyumba anayohama. Mpangaji mpya atakayekuja atajua mwenyewe! Huyo ndio Mwafrika, ingawa si wote, hata ukimchanja kwenye damu yake, utakuta chembe chembe za ushamba uliochanganyika na hila.


Hakika, hizo ni hulka za Mwafrika, hata azaliwe na kukulia Ulaya au Marekani. Si tumesikia majuzi, Waziri aliyepoteza ubunge alihakikisha anahamisha mpaka pazia kutoka kwenye ofisi ya mbunge jimboni kwake. Naambiwa, kuwa Waziri huyo kakulia Marekani. Kumbe, kukulia Marekani hakumwondolei Mwafrika hulka zake! Na hilo Ni Neno La Leo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.