MTANGAZAJI

MAISHA BORA KWA MTANZANIA???!!!!

Nimejaribu kuwanaliangalia hili neno "maisha bora kwa mtanzania" kwa uelwa wangu mdogo ni kama tusi au kejeli kwa kiongozi wa serikali kuliongea mbele yangu.

Kuna wizara ya mipango nanini sijui au kama haipo ila najua iko wizara inae waziri atleast inafanya mipango ya mustakhabari wa maendeleo ya nchi yangu, kila siku wingu la umasikini linazidi kuwa jeusi na wahusika hawawajibiki.

Inawezekana maisha bora ni kulala kwenye nyumba nzuri, kuendesha gari zuri, kula vizuri.... nk.

Sawa lak9ini vinatoka wapi? Karume marehemu alijenga nyumba kwa ajili ya wananchi wake, kunasehemu siikumbuki jina watu wanapikia kuni ghorofani na nyumba hazijulikani rangi yake ya kwanza ilikua ni ipi.

Zilijengwa kwa nguvu ya wananchi huku kukiwa na ulazimishwaji ndani yake, leo ukienda ukamtoa yule mwananchi atalaani kama nini.

Tunapoongelea maisha bora ya mtanzania nilitegemea nisijengewe nyumba na serikali ila niwekewe mazingira bora ya kunifanya nishamiri kimaisha.

Ninaomba mtu aniwekee ufafanuzi juu ya kilimo kwanza. Kama nalo ni moja ya kuelekea kweye maisha bora ya mtanzania well labda japo sina uhakika kwani yalikuwepo maazimio yahusuyo kilimo miaka mingi sana na sidhani kama linakitu kipya toka yale yaliopita.

Hivi ukiniambia nilime, sawa utanipa matrekta ambayo nasikia yule SPONSOR wa harusi ya waheshimiwa wawili kadaka tenda kunakitu hapo? Mkulima wa karafuu lazima awe na sababu ya kulima kama utamuhakikishia kuwepo kwa soko na bei nzuri ya mazao yao, je lipo hilo?

Japo soko ni kitu muhimu kwa mkulima lakini barabara za kufika kule alipo zipo? Nchi ina njaa kwa sasa lakini mpanda kunachakula kingi sana halafu reli ndo tumeiua. Tatizo kubwa linakuja nikutoona mipango mizuri endelevu inayokwenda sambamba na neno lenyewe "maisha bora kwa mtanzania".

Sekta binafsi ni sehemu nzuri sana ya kuleta maendeleo kwa nchi, tunahangaika na wawekezaji wa nje wakati tunashindwa kuwafanya wawekezaji wa ndani kukua na kuleta ushindani.

Hivi migodi yote kweli ni sahihi kuwapa watu wa nje? labda migodi ni kitu kikubwa na haya mashirika yaliouzwa kinyemela.

Kama mwekezaji wa ndani hana msaada toka kwa serikali yake mwenyewe hayo maisha bora yanakujaje? Fikiria mtu kaweza kuanzisha kampuni, kajitahidi kakusanya human resources nzuri tu anatafuta fursa ya biashara anashindwa kwa kukosa mtaji.

Tanzania investment benki (TIB) ipo haina msaada wowote kwanza inanichefua sana utendaji wake. Nilitegemea kuwa nimekuja na wazo liko verypositive napata support ya serikali, hata kama nitachukua mtaji toka TIB wakaweka mtu wao wa kusimamia mapato ya kampuni yangu mpaka deni lao likaisha sijali lakini hata hilo linashindikana.

Watanzania wako very creative ila system mbovu kiasi kwamba wanakuwa nafrustrations halafu mtu anasimama na kunihubiria maisha bora kwa mtanzania.

Kuna haja kubwa sana ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye muundo wa ukusanyaji mapato kwani mapato mengi sana yanapotelea mikononi mwa watu na serikali kushindwa kutoa hudumua kwa wananchi.

Muundo wa vyombo vya usalama na sheria hautoi muelekeo mzuri wa hili neno "maisha bora kwa mtanzani" kama rushwa itandelea, sheria hazifuatwi ni ngumu sana.

Uendeshaji wa mambo kwa kuheshimu taaluma ni kitu kilichokwisha poteza kabisa maana, mfano rahisi waziri anapotoa agizo bara bara ziwekwe matuta, mtaalamu akatekeleza.

Nimeshangaa TANROAD wamekubali hilo pia, je sheria za barabarani zingekuwa zinafuatwa tungekuwa na hofu ya kupoteza maisha ya watu? Sipendi kusikia mtu anaongelea maisha bora kwa mtanzania kwani ni kejeli na hata aneliongelea hajui maana yake.

Jovias Mwesiga
wanabidii@googlegroups.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.