MTANGAZAJI

MUARGENTINA ATAKAYE PAMBANA NA CHEKA AFAHAMIKA

Cheka akiwa Mazoezini katika gym ya Simba Oil Morogoro

Bondia Enrique Areco wa Argentina ndiye atakayezipiga na Bingwa wa dunia wa uzito wa middle anayetambuliwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa cha UBO,Francis Cheka kwenye uwanja wa Uhuru desemba 19 mwaka huu huko jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Shirikisho la Masumbwi Tanzania PST Emmanuel Mlundwa alisema jana kuwa Cheka atawania ubingwa wa Kamisheni ya Dunia ya ngumi za kulipwa au World Boxing Commision WBC ambao unashikiliwa na Areco.
Mtandao wa www.boxrec.com umemwelezea Enrique Areco aliyezaliwa mwaka 1964 kuwa ameshinda mapigano 43 ambapo 13 ni kwa KO,akiwa amepoteza michezo 15 ambapo 6 ikiwa ni kwa KO na kutoka sare michezo 7
Mtandao huo pia unamwelezea Francis Cheka kuwa bondia huyo aliyezaliwa 1982 na kuanza kucheza mpira wa miguu akiwa kipa wa timu ya Nondo FC ameshinda mapambano 18 ambapo 12 ikiwa ni kwa KO na kupoteza 6 ikiwa ni kwa KO kwa michezo 3 na kutoka sare pambano moja.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.