MTANGAZAJI

MIJADALA YA WANABIDII:Halmashauri za Wilaya zinafanya kazi gani

Kuanzia leo blog hii itakuwa ikikuletea michango mbalimbali ya masuala yanayotuhusu maisha yetu ya kila siku katika nyanja mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.Na tunaanza na hii ya Christian Nicholas

Halmashauri za Wilaya zinafanya kazi gani?
Kuna kitu kwa kweli kinaniumiza sana,na wakati mwingine nashindwa kujua hiv hawa wanaowekwa kwenye halmashauri zetu za jiji,manispaa na wilaya ni watanzania gani? Au wamelelewa na kusoma hapa TZ au ni mamluki? Kama ni mamluki,mamluki gani nchi nzima halmashauri zetu sura zake zinashabiiana? Hivi kwa mara ya mwisho lin umefika ofisi za mkuu wa wilaya,mkoa,elimu ,mahakama nk?

Jamani WATANZANIA NI AIBU KUBWA! nimetembelea halmashauri za wilaya takribani 45 na jiji 3,mambo niliyoyaona ni aibu na tunahitaji kubadilika na kutanguliza U-TANZANIA KWANZA.

Ofisi za halmashauri zetu kwa kweli hazifai,ni vijumba tu vya ajabu ama vya kukodi au vilitumiwa na wakoloni zamani,mfano kuna halmashauri moja ukifika kama ni mgeni ukaonesha kuwa hii ndo ofisi ya DC au mahakama ya wilaya utashangaa na hutokubali kirahs kama ilivyotokea kwangu mpaka uone bango la ofisi hizi nyeti,lakini nje ya ofisi kuna magari yenye thamani ya mil 200 pesa za TZ yameegeshwa na yanatumiwa na waheshimiwa hawa bila wasiwasi!

Utashangaa wanapata wapi ujasiri huu wa kutembelea mashangingi wakati ofisi ni tope na mavumbi? Hivi nani mpangaji wa sera za halmashauri na serikali kuu? Hapa napo tunahitaji mwekezaji? Tunafanya nini? Au kwa vile tunajua after five years naachia ngazi so atakuja mwingine? Jamani ni aibu kubwa sana,ninakerwa sana na hili,hebu tumwogope MUNGU.

Nilitembelea Kenya kwa kweli utashangaa ofisi za DC na mahakama,ukifika unajisikia kweli upo kwa DC mbona tuna mawazo ya kimaskini mbele za watu lakini mioyoni tunajua siri yetu.

Kuna wizara moja ya mahusiano ya Umma wakati fulani iliongozwa na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru,kwa kweli ni wizara nyeti ingawa sijui kama bado ipo,inaweza kuwa watch dog na kioo cha halmashauri zetu cha jinsi ya kutengeneza mapato na kuondoa utegemezi na zaidi ya yote kuanzisha akiba za malengo.

Kama utakuwa na maoni ya kuchangia mada basi waweza toa katika blog hii ama kwa kuyatuma kupitia wanabidii@googlegroups.com

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.