MTANGAZAJI

HUYU NDIYE FRANCIS CHEKA BONDIA TOKA MOROGORO

Francis Cheka akiwa na mkanda wake wa ubingwa
Akiteta jambo na kocha wake Abdallah Salehe Komando
Huyu ndiye bondia Francis Cheka "SMG" toka Morogoro anayeshikilia ubingwa wa dunia wa Middle Weght wa International Circuit Boxing (ICB) kuna habari kuwa anapanga kurudiana na Japhet Kaseba bingwa wa mabara wa kickboxing aliyemsambalatisha hivi karibuni,je kuna haja hiyo kwa Cheka???(Picha na Juma Mtanda)

4 comments

Anonymous said...

Cheka achana na mapambano yasiyo na maana, huyo Kaseba ni mdogo sana kwako.Promoter wako akutafutie mapambano ya maana (kimataifa)na yenye pesa nzuri.Wahuni kina Kaseba watakuua bure maana hawataki kushindwa.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kaka Francis

John Mwaipopo said...

Cheka usiwachekee wahuni. chonde chonde chonde usisikilize mapromota wachonganish. pia usisikilize redio mbao chonganishi. boxing ni mchezo lakini kwa mwendo huu mnaouonyesha mchezo unataka ugeuzwe vita. watasema maneno oooh haniwezi, kabahatisha, aliroga ilimradi tu wakupate ulingoni na wao wapate pesa. tayali naona kambi ya kaseba ni wagomvi na washari. tulimuona yule mtu aliyeingia kumfanyia vurugu Cheka. tena nimesikia cheka anataka kupambana na kaseba katika hiyo kickboxing. chonde choncde baba kickboxing ndio mtaji wa kaseba. hana nguvu mikononi. achana nae. kilikuwa ni kizingiti ushakivuka angalia mbele kwenye ulaji. boxing ina muda utahitaji kula nguvu yako siku ze mbele.

Mashughuli said...

Hello Mtangazaji habari yako kwako nakupongeza kwa kazi nzuri sana na globu yako inapendeza nilikuwa naomba msaada mmoja tu je aliyekudesignia hii blogu yako nitampataje??? please nisaidie

Hellen

Mtazamo News . Powered by Blogger.