MTANGAZAJI

NGUO ZA MITUMBA BONGO

Nguo za mitumba zinaonekana kupendwa barani afrika hasa hapa Tanzania kutokana na baadhi ya nguo hizo kuuzwa kwa bei poa. Lakini kama unavyoona akina mama hawa wakichangua nguo aina hii ili wanunue je ni kweli kwamba nguo za mitumba aina hii ni sahihi kuzitumia???

4 comments

Anonymous said...

uuuuuum, kaka nguo kama hizi hazifai kuvaliwa...bora tushoneshe mpya...magonjwa kaka............

Anonymous said...

Yakhee, ubaya wa hizi nguo ni pale wanapo zivaa kwa nje. Wajua tena hao dada zetu, vya ndani vyavaliwa nje.
Lakini yote kheri.

Anonymous said...

Mtangazaji umefulia yaani hii picha hipo hapo wiki moja nawakati kuna matukio mengi Bongo ambayo wananchi walio ndani ya nchi na nje ya nchi wanaofuatilia blog hii wanataka kufahamu vp? au sasa hivi upo bize sana Gangamala na kaza buti

Halafu mbona unazungumzia wakina dada tu hujui kama wanaume nao wananunua nguo za ndani za mitumba kitu cha muhimu kama mwanahabari ni kuishawishi serikali na mamlaka husika kupiga vita uingizaji wa nguo za mitumba za aina hiyo maana hapa bongo tumekuwa kama kichwa cha mwendawazimu kwa bidhaa za mitumba zisizokuwa na ubora. huko tunapo kwenda itakuja mpaka miswaki ya mitumba

Anonymous said...

Ukweli ni kwamba nguo hizi za mitumba zinaathari kubwa katika jamii.Lakini serikali iliruhusu nguo hizi kuingia nchini kwaajili ya wale wasioweza kumudu kununua nguo za dukani.
Ushauri ni kwamba mtu anaponunua nguo kama hizi asjeakazivaa kabla ya kuzifua ikiwezekana hata kwa maji ya moto,kwani nguo hizi huwa zimetumiwa na watu,na wengine wao huwa na magonjwa ya ngozi.
kwa hiyo mi ushauri wangu ndio huo hasa kwa nguo za ndani.

Mtazamo News . Powered by Blogger.