MTANGAZAJI

UBINAFSI NI HATARI ????

Wananchi wa Mbagala wakiangalia mabaki ya mabomu yaliyolipuka.
Katika miaka ya hivi karibuni watanzania ninaowafahamu kwa muda mrefu toka nizaliwe na kukulia hapa nchini tumekuwa wakarimu sana katika nyakati za raha na shida lakini hali hii sasa inaanza kutoweka kabisa na inatuelekeza pabaya,hili nimeliona tena baada ya kutokea mlipuko wa mabomu kule Mbagala jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waathirika wa mlipuko wa mabomu kwenye kambi ya Jeshi laWananchi(JWTZ)kikosi cha 671 huko Mbagala wamesema ujanja,nakujuana vimetawala katika shughuli ya ugawaji wa misaada na hivyokutowafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.
Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu mmoja wa waathirika haoaliyejitambulisha kwa jina la Simon ambaye baba yake mzazi alipataugonjwa wa moyo(BP)kutokana mshituko wa mabomu uliosababisha nakubomoka kwa nyumba yao waliyokuwa wakiishi amesema wasimamizihawatendi kazi inavyopaswa kwani wanajinufaisha wao.
"Tunashukuru watu wamejitoa kutusaidia lakini wasimamizi wa hiyomisaada aibu hawatendi haki ni wizi mtupu mimi na familia tu wazimaila nyumba ndo imeathirika pia baba yetu BP iko juu mpakasasa"amesema
Amesema viongozi nyumba kumi na wale wa mitaa ambao wamekuwa wakiandika majina ya waathirika na kuyakata kabla ya kuyafikisha kwa maofisawanaogawa misaada hiyo na kupachika mengine ambayo si ya walengwa
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya TemekeBw.Mkumbo alikiri kupokea malalamiko kutoka kwa waathrika hao jinsimisaada inavyogawiwa kwa kushindwa kuwafikia baadhi ya walengwa.
Tangu jumatatu jumla ya familia 3,750 zilitarajiwa kupatiwa misaadaambapo kila familia ilipangiwa kupatiwa kilo 30 za mchele na kilo10 za maharage.
Mlipuko wa mabomu ulitokea April 29,mwaka huu kwenye kambi hiyo yajeshi la wananchi na kusababisha vifo vya watu 24 kati ya hao raia19,na watu 306 walijeruhiwa ambapo kaya 907 zilibaki bila makazi

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.