MTANGAZAJI

MCHUNGAJI LISSO HATUKO NAYE

Habari za kusikitisha nilizozipata asubuhi hii zinaeleza kuwa Mchungaji Lisso amefariki leo asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mchungaji Lisso ambaye alikuwa akiishi nyumbani kwake Kilakala,Morogoro aliwahi kuwa Mbunge wakati wa serikali ya awamu ya kwanza nchini Tanzania kabla ya kuwa mchungaji katika Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania.

Kwa maelezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa kanisa hilo kanda ya Mashariki mwa Tanzania(ETC) taratibu za mazishi na masuala yote ya msiba yatakuwa nyumbani kwa Marehemu huko Kilakala,blog hii itaendelea kukuhabarisha zaidi.

"KUMBUKA MIMI NA WEWE NI MAREHEMU WATARAJIWA "
------------------------------------------------------------------

Habari zilizoifikia blog hii hivi punde zinaeleza ya kwamba kwa kuwa baadhi ya watoto,ndugu na jamaa wa marehemu wako mbali na mkoa wa Morogoro na wengine nje ya nchi,Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya jumapili Mei 24 mwaka huu katika eneo la makaburi lililopo ndani ya viwanja vya makao makuu ya ofisi ya Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kanda ya Mashariki mwa Tanzania

3 comments

Anonymous said...

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Poleni wafiwa.

Mwema Jr said...

Natoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki, ndugu na jamaa wote...

Anonymous said...

Poleni na Bwana awape faraja wafiwa wote na kanisa kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu. Katika yote Mungu ni mwema.

Mtazamo News . Powered by Blogger.