MCH.LISSO AZIKWA LEO
Alizaliwa Oktoba 1,1921 katika familia ya Ibrahimu Lisso Chabhula Chikwara na Elizabeth Nyakwesi Machumu,alianza maisha ya kifamilia Novemba 24,1942 kwa kufunga pingu za maisha na Zebida Nyamambara Karilo akiwa na miaka 21 na binti miaka 12 na kufanikiwa kupata watoto 11 na waliohai ni 7 ambao ni Jaredi(Kamoga),Tumaini,Ellen,Rose,Margaret,Maiga, na Dorah.
Mara nyingi marehemu alipokuwa akiwapa ushauri watoto wake wakati wa uhai wake katika suala la changamoto za maisha aliwaambia "DONT QUIT FIGHT WITHIN".
Marehemu aliyeacha watoto 7,wajukuu 31 na vituu 9 baada ya kumaliza elimu yake ya shahada ya kwanza katika chuo cha Solusi nchini Zimbabwe amewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini na pia amekuwa mchungaji kwa muda usiopungua miaka 38 akiwaamewahi kuwa mwalimu katika shule za Bugema,Suji,Bwasi,Kibumai na Ikizu hapa nchini na pia aliwahi kuwa Mtafsiri na mhariri wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania.
LALA BABA TUONANE ASUBIHI NJEMA
Post a Comment