MTANGAZAJI

NEEMA TENGA NDANI YA STUDIO ZA AWR TENA


Aliyewahi kuwa Katibu Muhtasi na Mtangazaji wa Redio ya Waadventista Ulimwengu(AWR) idhaa ya kiswahili alitembelea hapa studio akiwa na mumewe toka Uingereza wanakoishi hivi sasa.Ndoa yao ilifungwa hapa nchini mwaka jana,blog hii inawatakia maisha ya amani na furaha tele.

1 comment

Unknown said...

Maduhu ; blogu imekaa sawa; napenda ile rangi samawati (ya blogu lako) na mandhari kem kem hasa za Morogoro niliposoma mwaka 1973-74! Mji kasoro bahari, walisemaga wenyeji. Blogu yako pia inaonyesha taswira mbalimbali nje na ndani ya nchi. Hili ni jambo zuri sana ambalo miaka niliyokuwa kijana tusingeweza hata kidogo kulifanya. Enzi zile (kama miaka 25 iliyopita) tulikuwa tukitegemea tu magazeti ( na mengi yalipigwa marufuku nchini) au redio. Nimependa unavyoonyesha watu wa kila aina na mada za kila sampuli. Pia nimehusudu kuwa huchanganyi changanyi lugha kama wanavyofanya baadhi ya wanablogu na waandishi wetu wengi siku hizi. Inakuwa kama hatujui Kiswahili sawasawa au Kiingereza barabara. Tunaandika Kiswahili kisha tunakichovyea tone la Kiingereza ndani kama vile kujionyesha au kujifaragua kuwa Kiswahili hakitoshi msamiati kumbe si kweli. Lugha hizi mbili aghalab zinajitosheleza (hususan Kiswahili chetu mama). Lazima tuzitenganishe la sivyo tunakua hatuna hakika kama tunakula ugali kwa mchicha na nyama au ugali kwa mchicha uliochanganywa na maziwa mtindi. Kwa wale walioshawahi kula (au wanaojua)Loshoro ya Wamasai hicho ni kitu kinachoeleweka; ila hapa nimetumia nahau tu.

Mtazamo News . Powered by Blogger.