MTANGAZAJI

SEMINA ELEKEZI-NAIROBI KENYA

Semina elekezi zinahitaji uwe makini kwa kusikiliza na si kuwa kama wajumbe wetu ambao tuliwapa ulaji wanapoamua kuupiga usingizi wakiwa kwenye lile jumba kule Dodoma,Tanzania
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ECD, Steven Bina akielekeza wajumbe

Steven Bina akikabidhiwa baadhi ya vitendea kazi na Rais wa Masuala ya Fedha wa Redio ya Waadventista Ulimwenguni(AWR),Dowell W.Chow

IPI NI BORA ZAIDI? Ndivyo wanavyoulizana Mkurungezi wa Mawasiliano wa Uganda- Field (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kenya-Union

Baadhi ya wajumbe wa semina elekezi

Wajumbe toka Vituo vya Redio na TV huko DRC na Burundi


Tangu jana niko hapa katika eneo la Adventist Hill,jijini,Nairobi,Kenya ambapo nahudhuria semina elekezi ya AWR www.awr.org katika kuhakikisha kuwa nakuwa mtangazaji ambaye anaenda na mabadiliko yanayoteka katika dunia hii yenye changamoto za utandawazi,semina hii imehudhuriwa na wajumbe kutoka Marekani,Tanzania,Kenya,Uganda,DRC,Ethiopia,Somalia,Rwanda na Burundi.
Jambo lingine la kufurahisha ambalo msikilizaji wangu unapaswa kulifahamu ni kwamba kutakuwa na semina elekezi nyingine ambayo itawakutanisha wataalamu na wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA)toka sehemu mbalimbali duniani itakayofanyika hahapa Nairobi,Kenya kiingilio cha semina hiyo itakayofanyika kuanzia August 14 hadi 17,2008 ni dola 100 za kimarekani.
Kwa maelezo zaidi tembelea www.gien.adventist.org semina hiyo ni kwa kila mdau wa TEKNOHAMA ,
!!!!!USIPANGE KUKOSA!!!!!

1 comment

ombui said...

Ni vyema kuona maafisa wa mawasiliano wa kanila la Kiadventista wanapiga hatua wawezavyo katika kutumia teknologia mpya. Swali tu, tovuti za makanisa katika afrika mashariki zimejazwa ujumbe wa Kristo na kama ndio, habari mpya iliwekwa tovutini mwisho lini???

Mtazamo News . Powered by Blogger.