UDHIBITI WA MITANDAO YA KIJAMII PAKSTAN
Serikali ya Pakistan imezitaka kampuni kubwa za mitandao ya kijamii kuchukua hatua dhidi ya akaunti zinazohusiana na makundi ya kigaidi, ikionya kwamba kutokushirikiana kunaweza kusababisha hatua kali za kisheria.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Talal Chaudhry, alisema akaunti nyingi kwenye mtandao wa X (awali Twitter) zinatoka Afghanistan, India na sehemu zingine, zikieneza maudhui ya kigaidi na kusaidia makundi yaliyopigwa marufuku. Alionyesha ushahidi na kusema wapiganaji wa kigaidi wanafaidi msaada kutoka nchi hizo.
Chaudhry anaelea Pakistan inatumikia kama "ukuta kati ya magaidi na dunia" na kuonya kuwa makundi yanayopanga mashambulizi dhidi ya Pakistan yanaweza hatimaye kutishia mataifa mengine. Pakistan imeshuhudia ongezeko la ghasia zinazohusishwa na Baloch Liberation Army (BLA) na Tehrik-e-Taliban Pakistan (TTP), huku TTP ikiwa na uhusiano na Taliban wa Afghanistan.
Viongozi wa Pakistan mara kwa mara wamekosoa Afghanistan na India kwa kuunga mkono makundi haya. Uchunguzi wa hivi karibuni umebaini akaunti 19 za X zikihusiana na magaidi kutoka India, na zaidi ya akaunti 20 kutoka Afghanistan, baadhi zikionyesha uhusiano na serikali ya Taliban. Chaudhry alionya kuwa Kabul si tu inalinda magaidi, bali baadhi ya vipengele vya serikali vinawasaidia kueneza maudhui ya chuki na vurugu dhidi ya Pakistan.
Majukwaa ya WhatsApp, YouTube, Telegram na Facebook yameanza kusaidia Pakistan kutambua akaunti zinazohusiana na maudhui ya kigaidi. Akizitaka kampuni za mitandao kufungua ofisi nchini Pakistan na kutumia akili unde (AI) kugundua na kuondoa akaunti zinazoshabikia magaidi au kueneza chuki.
Katika miaka ya hivi karibuni, Pakistan imepiga marufuku kwa muda YouTube, TikTok na X, ikishutumu kushiriki maudhui ya chuki, matusi na yaliyovunja maadili ya taifa. Mwaka huu, bunge la Pakistan lilipitisha muswada wenye mamlaka makubwa kwa serikali kudhibiti mitandao ya kijamii, ikiwemo kifungo cha jela kwa wale wanaoeneza habari za uongo.

.png)
Post a Comment