MTANGAZAJI

KUNA UHALISIA MGUMU WA AI - UNDP

 


Nyuma ya sherehe na ahadi nyingi za Akili Unde (AI), kuna uhalisia mgumu, ikiwemo jinsi teknolojia hii inavyoweza kuwaathiri watu waliokosa fursa katika dunia inayozidi kuendeshwa na data.

Ripoti mpya kutoka Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP), inaonya kuwa faida nyingi za AI huenda zikayanufaisha mataifa tajiri na hivyo inapaswa hatua zichukuliwe kutumia teknolojia hii kusaidia kupunguza pengo katika upatikanaji wa mahitaji ya msingi na ujuzi wa hali ya juu katika teknolojia za kisasa.

Ripoti hiyo inalinganisha hali hii na “Mpasuko Mkubwa” wa mapinduzi ya viwanda, ambapo baadhi ya nchi zilipiga hatua kubwa huku zingine zikisalia nyuma.

Maswali kuhusu jinsi kampuni na taasisi zitakavyotumia AI yanazua wasiwasi, hasa kutokana na uwezo wake wa kubadilisha au kuchukua nafasi ya baadhi ya kazi zinazofanywa na binadamu. Hata hivyo, wahakiki wanasisitiza kuwa, kipaumbele kikubwa ni kuhakikisha watu kwanza, pili teknolojia, kama inavyoelezwa na Michael Muthukrishna wa Shule ya Uchumi ya London.

Ripoti pia inabainisha hatari ya kutengwa kwa jamii zilizo na upungufu wa umeme, mtandao, elimu, au zinazoathirika na vita, migogoro ya kiraia na maafa ya hali ya hewa. Watu hawa wanaweza kuwa “wasioonekana” kwenye data, hivyo kupoteza fursa za maendeleo ya AI.

Hata hivyo, AI inaweza kusaidia wakulima, kutoa uchanganuzi wa haraka, kuboresha utabiri wa hali ya hewa, na kusaidia jamii zilizo hatarini. Lakini katika mataifa tajiri, matumizi makubwa ya umeme na rasilimali ya data vimeibua wasiwasi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

Masuala ya maadili, faragha na usalama pia yameibuka, ikiwa ni pamoja na matumizi ya deepfakes na mashambulizi ya kimtandao. Tofauti kubwa ya kiuchumi na upatikanaji wa rasilimali katika Asia-Pasifiki pia yanaonyesha baadhi ya nchi na hata maeneo ya miji ya nchi zilizopiga hatua wanaweza kusalia nyuma.

Philip Schellekens, mchumi mkuu wa UNDP kwa ukanda wa Asia-Pasifiki, anaonya kuwa bila kufungwa kwa mapengo haya, mamilioni ya watu wanaweza kutengwa kutoka katika uchumi wa kidijitali.

Ripoti inahitimisha kuwa uwazi, kanuni madhubuti, uwekezaji katika miundombinu ya kidijitali, elimu na mafunzo, ni muhimu kuhakikisha AI inatumika kwa njia ya haki na kuwasaidia wale walioko hatarini.

Ripoti inaleza lengo kuu, “ni kueneza upatikanaji wa AI ili kila nchi na jamii inufaike huku ikiwalinda walio hatarini zaidi.”

 Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya Akili Unde yanaongezeka kwa kasi duniani kote. Ripoti za hivi karibuni za Kampuni ya Microsoft zinaonyesha kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)  kwa kiwango cha 59.4%  cha wakazi wake wa umri wa kazi, inashikilia nafasi ya kwanza kwa matumizi ya zana za AI. Karibu naye ni Singapore, na Norway, Ireland, na Ufaransa  pia zikiwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa matumizi ya teknolojia hii.

Nchi zenye idadi kubwa ya watu kama China na India zimeonyesha ukuaji wa haraka wa AI, hasa katika sekta za biashara, elimu, na huduma za umma. Baadhi ya nchi ikiwemo, Marekani na Korea United States, South Korea, na Taiwan, pia ziko juu kwenye orodha ya matumizi ya AI.

Watafiti wanasema tofauti hizi zinatokana na vipimo mbalimbali, miundombinu ya kiteknolojia, uchumi wa nchi husika, pamoja na sera zinazounga mkono uvumbuzi wa teknolojia. Hata hivyo, Microsoft inaeleza kuwa bado kuna nchi nyingi, hasa barani Afrika na sehemu za Asia ya Kusini, ambazo zinakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa AI.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.