MTANGAZAJI

VITUO VYA BUNIFU ZA TEKNOLOJIA VYAONYESHA UKUAJIA AFRIKA

 


Mwaka 2025 umeonesha maendeleo ukuaji wa  sekta ya teknolojia Afrika ambapo vituo vya bunifu za teknolojia za kisasa (Startups)  barani humo vimekusanya dola bilioni 1.35 katika miezi sita ya kwanza, ambalo ni ongezeko la 78% ikilinganishwa na mwaka 2024.

Miji ya Lagos, Nairobi, Cape Town, Johannesburg, Cairo, Accra, na Kigali ni vituo vya maendeleo kutokana na ufadhili, miundombinu na vipaji vya vijana kwenye teknolojia za kisasa.

Lagos inaongoza katika fintech na startups 503, thamani ya dola bilioni 9.8; startups 116 zimekusanya dola bilioni 6.03 tangu 2020. Nairobi, kama kitovu cha Afrika Mashariki, startups zilipokea dola milioni 638 mwaka 2024, asilimia 29 ya ufadhili Afrika. Cape Town na Johannesburg zinajikita kwenye cleantech, fintech, AI, na sekta za fedha. Cairo ni nyota kwa Afrika Kaskazini na ina thamani ya dola bilioni 8.3, startups 280 zikipata dola milioni 228 mwaka 2025.

Accra inakuza AI, medtech, agtech, na nishati mbadala; Kigali imekusanya zaidi ya dola bilioni 1 kupitia startups 55, ikijenga miradi ikiwemo Kigali Innovation City yenye thamani ya dola milioni 300.

Uwekezaji wa mitaji ya teknolojia  umeshuka 52% kati ya 2022 na 2024. Kenya, Nigeria, Afrika Kusini, na Misri zilipata asilimia 83 ya ufadhili robo ya kwanza 2025; fintech ikipata asilimia 46 ya uwekezaji.

 Huduma za 3G zimefikia 84% mwaka 2021, 4G 63%, na kasi ya intaneti imeongezeka hadi 8.31 Mbps mwaka 2022. Gharama za data zimepungua kutoka asilimia 11.5 mwaka 2019 hadi 5.7 mwaka 2021.

Miji ya Nairobi, Cape Town, na Stellenbosch inaongoza kwa vipaji vya teknolojia. Microsoft ADC Nairobi inashirikiana na vyuo kutoa mafunzo. Serikali zinaongeza vivutio kama punguzo la kodi na utafiti.

Changamoto za mabadiliko ya thamani ya sarafu bado zipo; Ghana ilipoteza asilimia 54 ya thamani ya cedi mwaka 2022. Uwekezaji wa kimataifa unachangia asilimia 80 ya mtaji, huku uwekezaji wa ndani ukizidi kukua.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.