MTANGAZAJI

MTANZANIA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAREKANI

 

Ndoto za kutafuta maisha nchini Marekani kwa Mtanzania Altman Mnyuku (kushoto kwenye picha) aliyekuwa akiisha South Bend, Indiana nchini humo zimekatishwa ghafla baada ya kupoteza maisha kutokana na kupigwa risasi alfajiri ya Julai 31, mwaka huu.
 
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania Waadventista Waishio Marekani (TAUS) kanda ya Midwest, Mch Emmanuel Sumwa kwa wanachama wa Umoja huo imeleza kuwa Altman alikuwa akitoa huduma ya usafiri wa Uber ambapo aliwachukua watu wanaosemekana kuwa wahalifu huko Chicago waliojaribu kumnyang'anya gari lake, katika kubishana na kushangaa kilichokuwa kikiendelea ndipo alipopigwa risasi ya shingoni, kisha watu hao walishuka kwenye gari wakakimbia.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.