MTANGAZAJI

VIONGOZI WA KANISA LA METHODISTI UINGEREZA WACHUNGUZWA

 


Uchunguzi wa sehemu mbili tofauti unaendelea kuhusu malalamiko dhidi ya  viongozi wakuu katika Kanisa la kimethodisti nchini Uingereza.
Uchunguzi huo ni kuhusu Mchungaji Graham Thompson, Rais wa Konferensi ya Methodisti, na Anthony Boateng, Makamu wa Rais, ulifichuliwa katika ripoti ya gazeti la The  Times.
Boateng anachunguzwa kutokana na  malalamiko kuhusu tabia yake na amesimamishwa kazi.
Mchungaji Thompson anachunguzwa kuhusu usimamizi wake na kushughulikia madai yaliyotolewa ndani ya kanisa lakini hajasimamishwa kazi, gazeti hilo linaeeza.
Boateng alidai kuwa hakujua malalamiko kuhusu tabia yake na alikanusha makosa.
Katibu wa Konferensi hiyo, Mchungaji Dkt Jonathan Hustler, alithibitisha uchunguzi huo na kuomba maombi katika ujumbe kwa waumini wa kimethodisti.
Anasema “Makamu wa Rais kwa sasa amesimamishwa kazi, lakini nisisitize kuwa kusimamishwa kazi ni kitendo kisichoegemea upande wowote na kipo ili kuwezesha uchunguzi kukamilika,”
"Itakuwa haifai kutoa maoni yoyote zaidi juu ya maelezo ya mambo haya; sasa tunahitaji nafasi na usiri kushughulikia maswala hayo haraka iwezekanavyo"
Habari za uchunguzi huo zinafuatia madai ya "mtazamo wa chuki dhidi ya wanawake na kilichoelezwa kuwa ni sumu" dhidi wanawake katika Kanisa, iliyofichuliwa katika ripoti ya ndani gazeti la The Times..
Ripoti hiyo ilidai kuwa kulikuwa na "maoni kuhusu mavazi, miguso isiyofaa, maneno machafu na tabia  za kudhalilisha wanawake, wakati mwingine za asili na wazi".
Pia ilikuwa na wasiwasi kwamba Kanisa la Methodisti nchini Uingereza "halikuonekana kama mahali salama" kwa  wanawake wengi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.