UTOAJI MIMBA CHANZO KIKUU CHA VIFO DUNIANI- WORLDOMETER
Takwimu zinaonyesha kuwa utoaji mimba ulikuwa chanzo kikuu cha vifo duniani kote kwa mwaka wa nne mfululizo, kwani idadi ya wanatoa mimba ilikaribia mara nne idadi ya vifo kutokana na magonjwa ya kuambukiza mwaka 2022.
Wordometer,Kanzidata inayofuatilia takwimu kuhusu afya, idadi ya watu Duniani na vipimo vingine kwa wakati halisi,imeendelea kukusanya taarifa kuhusu idadi ya utoaji mimba duniani kote.
Picha ya mwisho inayopatikana ya Worldometer kutoka 2022, iliyonaswa mnamo Desemba 31 na zana ya kuhifadhi kumbukumbu kwenye mtandao The Wayback Machine, inaonyesha kuwa zaidi ya mimba milioni 44 zilitolewa mwaka jana.
Wakati Worldometer inataja takwimu hizo kutoka kwa Shirika la Afya Ulimwenguni (WH)kama chanzo cha takwimu zake za utoaji mimba, WHO inashikilia kuwa "takriban mimba milioni 73 zinazotolewa hufanyika duniani kote kila mwaka,ambapo Shirika la kimataifa linadai kuwa utoaji mimba kama huduma muhimu ya afya.
Sababu ya pili kuu ya vifo mnamo 2022, kama ilivyotambuliwa na Worldometer, ilikuwa magonjwa ya kuambukiza, ambayo yalisabisha karibu watu milioni 13 waliugua magonjwa hayo.
Vifo vinavyotokana na magonjwa ya kuambukiza, pamoja na vifo zaidi ya milioni 8 vinavyosababishwa na saratani, vifo takriban milioni 5 vilivyosababishwa na uvutaji sigara, karibu vifo milioni 2.5 vinavyotokana na pombe na takribani vifo milioni 2 vilivyosababishwa na UKIMWI mwaka 2022 kwa pamoja chini ya idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na utoaji mimba mwaka wa 2022.
Sababu nyingine za vifo zilizotambuliwa na Worldometer ni pamoja na vifo vya ajali za barabarani, ambazo ziligharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 1 mwaka jana, na kujiua, ambayo ni zaidi ya milioni 1.
Zaidi ya watu 800,000 walipoteza maisha kutokana na magonjwa yanayohusiana na maji mwaka jana, watu nusu milioni walikufa kwa sababu ya homa ya msimu, karibu watu 400,000 walikufa kwa malaria na karibu wanawake 300,000 walikufa wakati wa kujifungua.
Idadi ya utoaji mimba uliofanywa mwaka wa 2022 ni ongezeko kidogo kutoka takriban milioni 44 zilizopimwa mwaka wa 2021.Karibu mimba milioni 44 zilitolewa mwaka wa 2020, ambapo mimba milioni 42.4 zilitolewa mwaka wa 2019. Katika miaka hiyo yote, utoaji mimba ulikuwa sababu kuu ya vifo duniani kote.
Post a Comment