MTANGAZAJI

DHORUBA YA MAJIRA YA BARIKI YAIKUMBA MAREKANI

 


Dhoruba kubwa ya majira ya baridi kali iliyovuma Magharibi mwa Marekani  ilimwagika hadi futi 4 za theluji katika sehemu za Nevada na Idaho, ilichochea maonyo ya theluji katika majimbo mengine sita na kusababisha vimbunga vilivyojeruhi takriban watu watano Kusini mwa Marekani.


Zaidi ya Wamarekani milioni 25 walikuwa katika tahadhari ya  hatari wa hali ya hewa  Jumanne. Mfululizo wa  dhoruba nchini kote kunaweza kudumu hadi mwisho wa juma ambapo sehemu  za kaskazini-mashariki zinaweza kupata ongezeko la zaidi ya futi moja ya theluji, watabiri wa hali ya hewama wameonya.


"Hii ni dhoruba ya 'hatutanii' ," Idara ya Usafiri ya Dakota Kusini ilituma ujumbe wa Twitter huku ikionya kuhusu kufungwa kwa barabara katika sehemu kubwa ya jimbo hilo. Onyo la Upepo wa baridi, Dhoruba ya theruji na utelezi vimetolewa. Mvua/baridi ya mvua na theluji kubwa pamoja na upepo mkali vitaathiri usafiri."


Sehemu za Nebraska, Colorado, Dakota Kusini, Montana, Wyoming na Kansas (Kensas) zilikabiliwa na hali ya kimbunga cha theluji - theluji yenye upepo wa angalau mile 35 kwa saa , na hivyo kupunguza mwonekano hadi robo ya maili au chini ya hapo - na majimbo mengine kadhaa yalikabiliwa na dhoruba ya msimu wa baridi na maonyo ya dhoruba ya barafu. , Huduma ya Taifa  ya Hali ya Hewa ilieleza.


Idara ya Usafirishaji ya Nebraska ilifunga sehemu za kati ya Barabara kuu nambari  80 na nambari 76. Doria ya Jimbo la Nebraska iliwahimiza watu kutotumia barabara.No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.