MTANGAZAJI

AMAZON KUPUNGUZA WAFANYAKAZI WAKE


 

Kampuni ya Amazon inapanga kuachisha kazi takriban wafanyakazi 10,000 katika kile ambacho kitakuwa punguzo kubwa zaidi katika historia ya kampuni hiyo ya Marekani. 

Ripoti ya Gazeti la New York Times imeeleza kuwa uondoaji wa wafanyikazi kwa wingi unaweza kuanza juma hii na utazingatia vitengo vya vya Amazon, kwa idara ya bidhaa zarejareja na rasilimali watu, likiwataja watu wenye ujuzi wa hatua hiyo ambao hawakuidhinishwa kuzungumza hadharani.

Taarifa ya Kuachishwa kazi  kunaweza kuathiri takriban 3% ya wafanyakazi wa walioko makao makuu ya kampuni ya Amazon na chini ya 1% ya wafanyakazi wake Duniani. Kampuni hiyo ina wafanyakazi zaidi ya milioni 1.5 duniani kote.

Ripoti ya hivi karibuni  kutoka kwa kampuni ya uchambuzi wa soko ya Finbold iligundua kuwa Amazon ilikuwa imepoteza 45% ya thamani yake katika mwaka uliopita, kutoka $ 1.6 trilioni Januari 1 hadi $ 939 bilioni Novemba 3. Makampuni mengine, ikiwa ni pamoja na Apple na Microsoft, pia iliona kushuka kwa thamani. 

Petra Moser, Profesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha New York, anasema  hasara ya thamani ya soko pengine ingeonekana kupitia ajira.,'Huu ni wakati mgumu': Amazon, Apple, makampuni makubwa ya teknolojia yanapoteza mabilioni ya thamani huku soko likiyumba.

 Jeff Bezos: Bilionea na mwanzilishi wa Amazon anasema anapanga kutoa sehemu kubwa ya mali yake kwa mashirika ya misaada.

Kampuni zingine kubwa za teknolojia nchini Marekani  zimetangaza hatua za kuwaachisha kazi watu  hivi karibuni, Maelfu ya watu waliachishwa kazi kwenye Twitter mwanzoni mwa Novemba, juma  moja baada ya bilionea Elon Musk kuinunua  kampuni hiyo.

Siku chache baadaye, kampuni mama ya Facebook ya Meta ilitangaza kuwa itapunguza wafanyikazi zaidi 11,000, karibu 13% ya wafanyikazi wake, "ili kuwa  yenye ufanisi zaidi katika kazi."

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.