MTANGAZAJI

UTAFITI: WASIWASI WA NDOA ZA SHINIKIZO LA FAMILIA AU JAMII

 

 

Wanandoa wanaofunga ndoa kutokana na shinikizo la kifamilia au kijamii wako katika hatari ya kufikia 50% zaidi, ya kuwa na ndoa ambayo huisha kwa talaka, kulingana na utafiti wa hivi karibuni kutoka Taasisi ya Ndoa ya nchini Uingereza (MF)

Utafiti huo uliopewa jina la "Mitazamo kuelekea ndoa na kujitolea," uliochapishwa mnamo Oktoba, uliwauliza watu wazima 2,000 ambao wamewahi kuoa ni kiasi gani walikubaliana au kutokubaliana na kila moja ya sababu 12 zilizowasilishwa na watafiti kwa nini walifunga ndoa.

Ili kuhakikisha kwamba matokeo yalikuwa muhimu kwa familia za leo, watafiti walilenga wanandoa 905 kutoka kwa sampuli ambazo walifunga ndoa kwa mara ya kwanza baada ya mwaka wa 2000 wakati uchumba wa mtandaoni ulipoibuka.

Wahojiwa ambao walisema "walihisi lazima waoe kwa sababu ya shinikizo la familia" walisajili uwezekano mkubwa zaidi wa talaka kwa 34% tu ikilinganishwa na 23% ya wanandoa ambao hawakutambua sababu hizi.

Utafiti huo unabainisha kwa njia nyingine, wanandoa ambao walifunga ndoa kwa sababu ya shinikizo la familia walikuwa na uwezekano wa 50% kutengana.

Wahojiwa ambao walikubali kwamba ndoa yao "ilitokea tu " pia ilikuwa na uwezekano wa 29% wa talaka katika muda wa utafiti ikilinganishwa na 22% ya wale ambao hawakukubali.

Watafiti pia waligundua kuwa harusi zenye maandalizi ghali yanayogharimu zaidi ya £20,000 karibu Shilingi milioni 52 za Tanzania , kukutana mtandaoni au kazini badala ya kukutana na familia na marafiki, na kuwa na wageni wasiozidi 10 kwenye harusi yote yalihusishwa na hatari kubwa ya talaka katika miaka ya mwanzo ya ndoa.

Utafiti unaonesha kuwa Watu ambao hufunga ndoa kwa  msingi wa kujenga maisha pamoja kwa ujumla walifanya vizuri zaidi kuliko wale waliofunga ndoa kutokana na shinikizo la kijamii.
No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.