MTANGAZAJI

ATHARI ZA UVIKO-19 KWA MAKANISA MAREKANI

 


Takribani miaka mitatu baada ya kuondolewa kwa karantini ya janga la Covid-19 ya kulazimisha makanisa nchini Marekani kufunga milango yake kwa ibada, waumini wengi bado hawajajitokeza kuhushduria kwenye makanisa ingawa huduma zimerejea kama ilivyokuwa zamani.

Utafiti wa kituo cha Lifeway umetoa matokeo ya uchunguzi wa simu wa wachungaji 1,000 wa Kiprotestanti uliofanywa kuanzia Septemba 6 hadi Septemba 30, 2022, kwa kutumia sampuli kutoka kwa orodha ya makanisa yote ya Kiprotestanti.Kila mahojiano yalifanywa na mchungaji Kiongozi  mhudumu au kasisi kanisani, na majibu yalipimwa kulingana na eneo na ukubwa wa kanisa ili kuakisi idadi ya watu kwa usahihi zaidi.

Wachungaji wote waliohojiwa walisema makanisa yao yalianza ibada za kawaida mnamo Agosti 2022, ikilinganishwa na 75% walioripoti sawa mnamo Julai 2020.

Lakini wakati makanisa yanaanzisha tena huduma zao za ana kwa ana, kwa wastani, wachungaji wanasema nahudhurio katika makanisa yao mwezi Agosti ilikuwa 85% ya viwango vyao vya mahudhurio ya siku za Ibada kwa Januari 2020.

Kwa mujibu wa utafiti huo Kanisa la wastani liliripoti 63% ya mahudhurio yake ya ana kwa ana kabla ya janga hilo mnamo Septemba 2020. Kufikia Agosti 2021, idadi hiyo ilipanda hadi 73% na kuruka alama zingine 12 mnamo 2022.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.