MTANGAZAJI

GAiN ULAYA 2022 YAMALIZIKA

 

Zaidi ya wana mawasiliano 180 wa Kanisa la Waadventista wa Sabato wamekutana  Bucharest, Romania, kwa Mkutano wa wanamawasilino wa kanisa hilo (GAiN) 2022 barani Ulaya uliomalizika hivi karibuni.
Tukio hilo lililokuwa na kauli mbiu ya  "Mbele: Endelea Kusonga" lilikusanya viongozi wa mawasiliano na wataalam kutoka nchi 35 wanaofanya kazi katika Uandishi wa habari wa Kiadventista, Redio, TV, na mitandao ya kijamii.
Wengi wa wanamawasiliano  waliojiandikisha kwa GAiN Ulaya  wanahudumu katika eneo la Kanisa la Waadventista Katika Divisheni mbili za Bara hilo (EUD) na (TED). Baadhi ya washiriki hata hivyo  walitoka mbali ikiwemo  Polynesia, Mongolia, na Mexico.
Kundi la wanamawasiliano Waadventista kutoka Ukrainia pia waliendesha gari kwa saa nyingi ili kuhudhuria mkutano huo.
Awali mkutano huo ulipangwa 2020, lakini ilibidi uahirishwe kwa sababu ya janga la Corona,"Tunafurahi tunaweza kuifanya miaka miwili baadaye, tukiwa na watu zaidi," Mkurugenzi wa zamani wa mawasiliano wa EUD Corrado Cozzi alisema wakati wa hotuba yake ya ufunguzi Oktoba 14 huku akisisitiza kuwa walifanya matukio mawili ya mtandaoni, lakini haikuwa sawa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.