WANNE WAPOTEZA MAISHA BAADA YA NDEGE KUANGUKA
Watu wanne wamepoteza maisha baada ya ndege kuanguka karibu na uwanja wa ndege huko Califonia jumamosi Disemba 4,2021 mamlaka imeeleza.
Wafanyakazi wa idara ya Dharura walianza kutoa msaada baada ya kupokea simu baada ya saa 12:30 jioni kuwa ndege ndogo ilikuwa imedondoka chini karibu na uwanja wa ndege wa Visalia,Califonia
Wapelelezi kutoka Kitengo cha Polisi cha Tulare walikuwa katika eneo la tukio na kuendelea kuwepo hapo hadi jumapili ya Disemba 5,2021 walipofika maafisa wa Ndege wa serikali.
Ndege iliondoka uwanja wa ndege wa Visalia 12:37 jioni, Sanjenti Jesse Cox amesema,Baada ya dakika nne za kupaa kwa ndege hiyo walipokea simu kupitia namba ya dharura ya 911, kwa mujibu wa program tumishi inayofuatilia mwenendo wa ndege inaonesha kuwa Piloti wa ndege hiyo alijaribu kurudi uwanjani hapo baada tu ya kupaa kwa ndege.
Magari ya uokoaji na zimamoto walifika eneo ilipoanguka ndege hiyo kwa ajili ya kutoa msaada.
Post a Comment