WAMISIONARI WALIOTEKWA WAACHIWA HURU
Wamisionari wa mwisho 12 ambao walikuwa wametekwa huko Haiti wameachiwa huru,Shirika la Kikristo linalojihusisha na Huduma ya Misaada (CAM) ambalo liliwapeleka nchini humo limeeleza.
Kundi la Wamisionari 17 walitekwa Oktoba mwaka huu likiwa njiani kutoka katika huduma ya kutembelea Kituo cha Watoto Yatima cha CAM huko Haiti.
Wamisionari hao 16 wanatoka Marekani na mmoja Canada,ambapo pia lilijumuisha watoto na mdogo kuliko wote akiwa na miezi minane
Kikundi 400 Mawozo kilieleza kuhusika na utekaji huo ambapo lilitaka malipo ya fidia ya Dola Milioni moja za Kimarekani kwa kila mtu ili kuwaachia.
Kiongozi wa watekaji hao Wilson Joseph alitoa vitisho vya kuwaua wamisionari kama fidia ama la wangewaua wamisionari.Wawili waliachiliwa Novemba huku watatu wakiachiliwa mwanzoni mwa mwezi huu.
CAM yenye makao yake makuu huko Ohio imethibitisha Disemba 16,2021 kuwa kundi lote la Wamisionari wameachiwa huru.
Post a Comment