MTANGAZAJI

KIJANA MTANZANIA AFARIKI GHAFLA NCHINI MAREKANI

 

 Kijana wa Kitanzania Jason Mtsimbe mwenye umri wa miaka 24 aliyekuwa akiishi na Mama yake huko Chattanooga Tennesse nchini Marekani amefariki ghafla Disemba 22,2021.
 
Mama wa Jason Dkt Mbaki Onyango ambaye ni mhadhili katika Chuo Kikuu cha Tennesse ameeleza kuwa alimkuta mwanae chumbani asubuhi akiwa amefariki Dunia,ambapo usiku wa kuamkia siku hiyo waliongea na mwanaye kabla hajaenda kulala.
 
Marafiki,Ndugu,jamaa na Watanzania Waadventista waishio Marekani na Canada (TAUS) na nchi zingine Duniani wamekuwa wakikutana kila siku jioni kwa saa za Marekani kwa njia ya mtandao wa zoom kwa ibada ya faraja na kupanga mipango ya kusafirisha mwili kwenda Tanzania kwa mazishi mara baada ya taratibu za uchunguzi wa sababu za kifo cha kijana.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.