MTANGAZAJI

MOTO WATEKETEZA MAMIA YA NYUMBA MAREKANI

 


 
Maelfu ya watu wanaombwa kuhama mara moja huku  mamia ya majengo yameteketea ambapo  pepo zinachochea  moto wa nyika unaosambaa kwa kasi katika Kaunti ya Boulder huko Colorado nchini Marekani.
 
Taarifa ya Polisi wa Boulder imeeleza kuwa toka Alhamisi Alasiri kumekuwa na  Moto  mkali wa nyasi, uliochochewa na nyaya za umeme zilizokatika huku kukiwa na upepo mkali katikati mwa Colorado.
 
 Mkuu wa Polisi Joe Pelle aliwaambia waandishi wa habari kuwa moto wa nyika uliripotiwa kwa mara ya kwanza baada ya saa 11 asubuhi Alhamisi na tangu wakati huo umepungua kiasi ukiwa umeshaunguza ekari zipatazo  1,600 hadi Alhamisi jioni.
 
Louisville, Colorado, yenye wakazi wapatao 20,000, wakazi wake wametakiwa  kuhama kutokana na Moto huo, kwa mujibu wa  Ofisi ya Boulder ya Usimamizi wa Dharura. Jiji zima la Superior, Colorado, lenye wakazi wapatao 13,000, pia wakazi wake wametakiwa kuhama kutokana na moto huo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.