MTANGAZAJI

UTAFITI-WASEJA WAONGEZEKA MAREKANI


 Takribani watu wazima wanne kati ya 10 nchini Marekani wanaishi bila kuwa na wenzi,mwenendo unaoongezeka kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha Utafiti cha Pew (PRC)

Kwa kutumia taarifa za sensa,Pew ilibaini ripoti hivi karibuni kuwa asilimia 38 ya watu wazima nchini Marekani kwa mwaka 2019 walikuwa hawaishi na wenzi ambalo ni ongezeko kutoka asilimia 29 iliyoripotiwa mwaka 1990.

Asilimia 53 ya watu wazima mwaka 2019 walikuwa wameoana,ikiwakilisha kushuka kutoka asilimia 64 iliyoripotiwa mwaka 1990,wakati huo huo asilimia 6 ya watu wazima waliishi pamoja kwa mwaka 2019 kutoka asilimia 4 ya mwaka 1990.

Mtafiti Mwandamizi wa Pew ,Richard Fry na Mkurugenzi wa Masuala ya Jamii Kim Parker katika uchambuzi wao wanasema ongezeko la Idadi ya Waseja linasababishwa hasa kushuka kwa idadi ya ndoa hasa katika kipindi cha  umri wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi.

"Idadi ya  wasio na wenzi inajumuisha watu wazima ambao awali walikuwa wameoa na kuolewa na sasa wametengana,wametalakiana,wajane na wagane idadi ambayo imeongezeka toka mwaka 1990 ikijumuisha na wale ambao hawajaoa ama kuolewa"

Watafiti wamehitisha kuwa ongezeko la waseja limesababsha athari kubwa kwa  jamii,ikiwa ni pengo linalokua la ustawi kati ya watu wazima walio na wenzi wa maisha na waseja,jambo ambalo linasababisha matatizo ya kiuchumi katika familia,ukosefu wa elimu na msongo unaotokana na upweke.

 Januari 2020 kabla ya sheria ya Karantini ya Janga la Corona nchini Marekani,Kampuni ya Bima ya Cigna ilitoa utafiti ilioufanya kwa watu wazima 10,400 ambao ulionesha kuwa asilimia 61 ya watu hao walikuwa wapweke. 

Mwaka jana Taasisi ya Elimu ya Familia yaVirginia ilitoa ripoti ikionesha taarifa kutoka Wakala wa Sensa nchini Marekani-UCBACS ambayo ilionesha kuwa kulikuwa na kiwango kidogo cha watu wanaotalakiana wenye umri wa miaka 50 kwa mwaka 2019,Ambapo ripoti ilionesha kuwa kila ndoa  1,000 kati ya hizo ndoa 14.9 zilivunjika kwa mwaka huo.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.