MTANGAZAJI

GOOGLE KUWEKEZA DOLA BILIONI 1 AFRIKA

 

 

Kampuni ya Google imetangaza Oktoba 6,2021 uwekezaji wa Dola Bilioni Moja za Kimarekani  kwa kipindi cha miaka mitano ijayo ili kuruhusu ukuaji wa haraka wa mtandao wa Internet na upatikanaji wake kirahisi na pia kusaidia wajasiriamali wa Afrika.

“Leo nina furaha kutangaza mpango wa kuwekeza dola bilioni moja Afrika kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano. Itashugulikia juhudi kadhaa za kuboresha mungiliano wa uwekezaji. Uwekezaji huu utasaidia mabadiliko ya kidigitaji barani Afrika katika maeneo manne muhimu," kampuni hiyo imeeleza.

Kutegemea internet ni tatizo katika bara la Afrika ambapo chini ya theluthi moja ya watu Bilioni 1.3 wa Bara hilo wameunganishwa katika mtandao, hiyo ni kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Katika bara hilo ambapo karibu nusu ya idadi ya watu ni chini ya miaka 18 ndiyo soko la intaneti.

Pesa hizo kiasi cha  Sh115.2 bilioni ni kwa ajili ya kusaidia kampuni za ubunifu zinazochipukia zilizopo barani Afrika ili kuzisaidia kukuza biashara zao na kutoa suluhu kwa matatizo ya jamii. 

Kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya Sh2.3 trilioni za mfuko wake wa uwekezaji barani Afrika ambazo itazitumia kwa miaka mitano ijayo katika kampuni za teknolojia barani humo.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Alphabet Inc, kampuni ya mama ya Google, Sundar Pichai amesema lengo kutoa Sh115.2 bilioni ni kuinua biashara ndogo ndogo na startups ili kuongeza wigo wa biashara katika bara la Afrika.

Utoaji wa fedha hizo na mambo mengine unafanyika chini ya programu ya Google ya Startups Accelerator Africa 

Hadi sasa, Bunifu  50 zimechaguliwa kushiriki kwenye programu hiyo ya Afrika inayotarajiwa kuanza Oktoba 13 mwaka huu ambapo kila startup itapatiwa Sh230 milioni pamoja na mikopo kutoka programu za Google za ‘Google Cloud’ na ‘Google Ads’.

Kati ya Bunifu  50 zilizochaguliwa, asilimia 40 zinaongozwa na wanawake zikiwakilisha nchi tisa na sekta 12.

“Kuna pengo kubwa katika upatikanaji wa mitaji. Makundi mengine hayafikiwi na mitaji kama mengine. Tumeyaona hayo kwa startups zinazoongozwa na waanzilishi wanawake wenye asili ya Afrika,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Google wa nchi  za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Nitin Gajria.

Gajria amesema kuwa jitihada zinafanyika kwa ajili ya kuziba pengo hilo  na wameamua kuleta mitaji barani Afrika.

Licha ya kuwa Afrika ina nchi kubwa zilizoendelea kiteknolojia (Nigeria, Kenya, Afrika Kusini na Misri), kampuni hiyo imesema itaendelea kupokea maombi kutoka kwa startups hata katika nchi ambazo hazifikiwi na mitaji hiyo.

Nchi hizo ni pamoja na Algeria, Botswana, Cameroon, Ivory Coast, Ethiopia, Ghana, Morocco, Rwanda, Senegal, Tanzania, Tunisia, Uganda na Zimbabwe.

“Hatufungamani na nchi zozote. Tumeweka umakini wetu kwenye kuwekeza kule tunaamini Google itaongeza thamani,” amesema Gajria.

Google ambayo imekuwa ikisaidia kampuni changa kupitia Mfuko wa Uwekezaji Afrika kwa miaka mitatu sasa, imefikia Bunifu  80 mbalimbali barani Afrika zikiwemo Twiga, Paystack na Piggyvest.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.